• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Mrejesho |
    • Lalamika |
Musoma Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Wasifu wa Kijamii na Kiuchumi wa Halmashauri
      • Viongozi wetu
        • Mayors
        • Municipal Directors
    • Dira na Dhamira
    • Maadili yetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Rasilimali Watu na Utawala
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Idara ya Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Idara ya Mipango Miji na Ardhi
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Usafishaji na Mazingira
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria na Usalama
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Teknolojia, Habari, Mawasiliano na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Maeneo ya Viwanda
    • Usafirishaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za maji
    • Maombi ya Huduma
    • Uthibi wa Mazingira
    • Uthibiti wa Misitu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha na Uongozi
      • Kamati ya Elimu, Afya na Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Mipango Miji na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
      • Kamati ya Maadili ya Madiwani
    • Ratiba ya vikao
  • Miradi
    • Miradi inayopendekezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mwongozo wa kushughulikia Malalamiko
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Wasifu wa Kijamii na Kiuchumi wa Halmashauri
    • Miongozo na Nyaraka
    • Sheria ndogo
    • Majarida
    • Council Budget
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba
    • Makala

Uhifadhi wa Mazingira

Imewekwa: August 31st, 2018

Mlima Mukendo Mbioni Kuwa Eneo Lindwa

Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba ameridhia ombi la Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kuufanya mlima Mukendo kuwa eneo lindwa.

Mlima Mukendo unaopatikana katika Mtaa wa Nyerere Kata ya Mukendo Una eneo la mita za mraba 101,974 sawa na ekari 25 au hekari 10. Mlima huu uko umbali wa takribani km 1 kutoka kituo cha mabasi cha mjini.

Awali akisoma taarifa ya uhifadhi wa mlima Mukendo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa Mkuu wa idara ya Mazingira na Uthibiti wa taka ngumu Bw. Dotto Tambuko alieleza sababu zilizopelekea kutaka mlima huo kutangazwa kama eneo lindwa ni uwepo wa uoto wa asili ambao unasaidia kurekebisha hali ya hewa ya Musoma.

Aliongeza kuwa Mlima huu una wanyama wengi hasa wanyama wadogo wadogo na ndege ambao wako katika hatari kubwa ya kuharibiwa kutokana na shughuli za binadamu za kiuchumi na kijamii.

Sababu nyingine ni kama Mimea ya Mlima Mukendo inaondolewa kwa kasi kubwa kuliko inavyorudishiwa, Kuna shughuli zingine za matumizi ya ardhi kwenye eneo hilo inayoweza kusababisha uharibifu wa mazingira pamoja na Mlima Mukendo ukihifadhiwa unaweza kuwa moja ya vivutio muhimu kwa watalii (ecotourism).

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. William Gumbo akimkaribisha waziri  Makamba kutoa hatuba alitoa ombi maalum kwa waziri kuwa hatua zote za utangazaji wa eneo hilo zisiathiri hali ya sasa ya mlima ikiwa ni pamoja na taasisi pamoja na miundombinu iliyopo kwa kuwa ina historia ya pekee ya mlima huo.

Kwa upande wake Waziri Makamba alipongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Manispaa katika uhifadhi wa mlima Mukendo na kutaka jitihada hizo kuungwa mkono na wapenda mazingira na wananchi wote kwa ujumla.

“Mnafanya kazi ya kuitunza hadhi na heshima ya Musoma kwa kutunza mazingira” alisema Makamba  na kuongeza kuwa “Sisi kama wizara tunandaa masharti ya uhifadhi wa mlima Mukendo na matumizi ya mlima” .Alisisitiza.

Makamba alisifia mandhari ya mlima na kusema ” Mji wa musoma umejaliwa kuwa na ziwa hivyo kuufanya kuwa maalum hasa ukingatia mandhari nzuri ya mlima huu tuliopo. Ukiwa hapa unauona mji wote wa musoma pamoja na ziwa Victoria’’. Alisema.

Akitoa shukrani kwa waziri Makamba mkuu wa wilaya ya Musoma Mhe. Vicent Naano alisema Wilaya ya Musoma imejipanga ipasavyo kutunza na kulinda mazingira kwa kupanda miti Mil. 10 ndani ya miaka 5.

Mlima Mukendo upo katika hatua za mwisho za kutangazwa kama eneo lindwa kutokana na kukidhi vigezo vilivyowekwa na serikali ili eneo litangazwe kama eneo maalum linalohitaji kuhifadhiwa na kulindwa.

Matangazo

  • Tangazo la matokeo ya zabuni ya ujenzi wa barabara za lami Mjini February 17, 2017
  • mikataba ya zabuni iliyotolewa kwa mwaka wa fedha 2015-2016 na 2016-2017 August 01, 2017
  • Matokeo ya Ununuzi wa Gari la Taka September 12, 2017
  • Tangazo la Zabuni za Mapato September 12, 2017
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Magufuli Aikumbuka shule aliyosoma Hayati Baba wa Taifa

    September 06, 2018
  • Siko tayari Watanzania wanyanyasike

    September 05, 2018
  • Magufuli aitangaza Mara kama mkoa wa ukombozi

    September 05, 2018
  • Makamba asisitiza utunzaji wa Mazingira

    September 01, 2018
  • Tazama zote

Video

Hotuba ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara
Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sisi ni nani
  • Dira na Dhamira

Viunganishi Linganifu

  • IKULU
  • Public Service Management
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Musoma Municipal Council

    Sanduku la Posta: Box 194 Musoma

    Simu: 0282622560

    Simu ya Mkononi: +255755215348

    Barua pepe: info@musomamc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2017 GWF . All rights reserved.